Mwishoni mwezi wa kwanza mwaka huu mtandao wako wa Teknokona ulikuletea habari juu ya Facebook kuleta video za moja kwa moja yaani live, leo tunakufahamisha kwamba sasa huduma hii inapatikana kwa watumiaji wote wa Facebook duniani kote.
Hii ni fursa kwa watumiaji mbalimbali wa Facebook ambao watazitumia vizuri video za moja kwa moja ili kuwashirikisha marafiki zao matukio ambayo hawakuweza kuwapamoja nao kaitika jambo fulani.
Hili ni pigo kwa mitandao mingine ambayo ilikuwa ikitoa huduma ya video za moja kwa moja kama vile Youtube na Periscope ya Twitter, Umaarufu wa Facebook unaipa nafasi kubwa ya kutawala soko la huduma hii na hivyo kuwa tishio kwa mitandao ambayo ilikwisha anza kutoa huduma hii.
Tayari tumekwisha ona mitandao kama vile Snapchat ikipata umaarufu mkubwa kwa kutumia huduma za video, hii ni ushaidi tosha kwamba mitandao ya kijamii inaelekea upande wa video za moja kwa moja. Mapinduzi ya speed za intanet pia ujio wa teknolojia za 4G pamoja na kushuka kwa gharama za intaneti ni moja ya vichochezi vya mambo haya.
Kwa hapa kwetu Afrika mashariki tutegemee zaidi kuona shughuri kama mikutano ya siasa, dini na hata sherehe ndogo ndogo kama za kuazimisha siku ya kuzaliwa kuwa ndio hasa zinazorushwa katika huduma hii ya video za moja kwa moja. Ingawa wasiwasi wetu ni kwamba kunaweza kuwepo kwa utumiaji mbaya wa huduma hizi kama vile kurusha shughuri zisizo kubalika kijamii.
Yote kwa yote hii ni habari nzuri kwa Facebook ambayo sasa ipo katika nafasi nzuri kupambana na mitandao mingine inayokuwa kwa kasi.
SOMA ZAIDI: Facebook yaleta video za moja kwa moja