Mara nyingi mtandao wa kijamii wa WhatsApp umekua ikufuata nyendo za mtandao wa kijamii wa Telegram lakini sio katika hili.
Hapo awali mara kwa mara tulikua tukiona vipengele vingi katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp vilikua vinatumika toka zamani katika mtandao wa kijamii wa Telegram.
Kipengele cha View Once ni kipengele pendwa sana katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kinakua kama ni sehemu ya kulinda kwa kiwango cha juu taarifa zako kwa njia ya picha au sauti.
Telegram nao wameona wasibaki nyuma kabisa katika kipengele hiki katika huduma ya sauti na video kwa upande wa meseji.
Ndio kipengele hiki sio kipya kabisa katika mtandao huu na hapo awali kilianza kutumika katika picha na video peke yake na hii ni katika mazungumzo ya watu wawili.
Kumbuka kwa mara ya kwanza kabisa kipengele hiki kilianzishwa mwezi septemba mwaka 2023 na mapokeo yake yakawa mazuri na kwa sasa kuna maboresho zaidi.
Inamaana kwa haraka haraka kwa sasa watumiaji wa mtandao huu wana uwezo mkubwa wa kusikilia sehemu ya kurekodi sauti (voice note) na kisha kuachia wakishamaliza kurekodi sauti hiyo na kisha kuchagua eneo la ‘view once’
Hili linawezekana hata katika kipengele cha jumbe za video…ukishamaliza kurekodi jumbe yako unachagua chaguo hilo hilo la ‘view once’
Pia Telegram imeweka uwezo wa kusimamisha kwa muda (pause) jumbe hizo za video na sauti.
Ni kawaida kwa mtandao huo kuja na maboresho kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata kile kilichobora zaidi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani mtandao wa Telegram utaupita mtandao wa WhatsApp kwa idadi ya watumiaji? Niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.