Jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama wa barabarani kitaanza kutumia teknolojia ya kisasa zaidi kwa ajili ya kurekodi makosa ya madereva barabarani na pia ya kurahisisha ufanyaji wa malipo ya faini zitokanazo na makosa hayo.
Jisomee kwa maelezo zaidi na kisha tuambie mawazo yako.
KUANZA KUTUMIKA KWA KANUNI MPYA ZA
I. TOZO LA PAPO KWA HAPO KWA NJIA YA KIELETRONIKI (THE ROAD TRAFFIC (NOTIFICATION OF OFFENCES) (AMENDMENT) REGULATIONS, 2015, NA
II. KANUNI YA KUWEKA NUKTA KATIKA LESENI ZA UDEREVA (THE ROAD TRAFFIC (DRIVERS LICENSE POINT SYSTEM) REGULATIONS, 2014.
1. KANUNI YA TOZO LA PAPO KWA HAPO KWA NJIA YA KIELETRONIKI.
Kanuni hii ni ya Sheria ya Usalama Barabarani inayohusu ulipaji wa tozo la papo kwa hapo kwa njia ya kielektroniki. Kanuni hii inasomwa pamoja na Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168 kama ilivyorejewa mwaka 2002, Kifungu cha 95 Iliyotiwa saini na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kupewa namba 30/2015 kisha kutangazwa katika gazeti la Serikali la tarehe 30/01/2015. Kanuni hii itatumika katika kulipisha faini za papo kwa hapo kwa njia ya mtandao.
Ndugu Wanahabari,
Kutokana na kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa wamiliki wa magari na madereva kwamba wamekuwa wakilipishwa faini na askari barabarani pasipo kupewa risiti halali za serikali (GRR), Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau liliamua kubuni mfumo wa kielektroniki utakaochukua nafasi ya mfumo unaotumika sasa wa tozo la papo kwa hapo.
Mfumo huu utaanza kwa majaribio katika baadhi ya maeneo tu (Live testing) Jijini la Dar es salaam kuanzia kesho Alhamisi tarehe 17/09/2015. Hivyo msishangae kuwaona askari wakiwa barabarani na mashine zitakazotumika katika ulipishaji wa faini za papo kwa hapo.
Ni matumaini yetu kwa kuanzia na Jiji la Dar es salaam itatusaidia kubaini changamoto zitakazojitokeza na kuweza kuja na mfumo bora zaidi tutakapoanza nchi nzima.
Ndugu Wanahabari,
Mfumo wa ulipaji faini za papo kwa hapo kielekitroniki unafanyakazi kama ifuatavyo:
Dereva aliyetenda kosa akikamatwa na kutakiwa kulipa faini kwa njia ya kielektroniki, askari ataingiza kwenye mashine taarifa za namba ya usajili wa gari, nambari ya leseni ya dereva, eneo kosa lilipofanyika, kosa lililofanyika na kisha askari atatoa tiketi ya kielektroniki kumpa dereva aliyetenda kosa.
Mfumo wa ulipaji faini za papo kwa hapo kielekitroniki unafanyakazi kama ifuatavyo:
Dereva aliyetenda kosa akikamatwa na kutakiwa kulipa faini kwa njia ya kielektroniki, askari ataingiza kwenye mashine taarifa za namba ya usajili wa gari, nambari ya leseni ya dereva, eneo kosa lilipofanyika, kosa lililofanyika na kisha askari atatoa tiketi ya kielektroniki kumpa dereva aliyetenda kosa.
Tiketi hiyo pamoja na kuwa na namba ya kumbukumbu ya malipo pia itakuwa na maelekezo kwa dereva yanayosema: Unatakiwa kulipa faini ya kosa ulilotenda kupitia mitandao ya simu ya tigo pesa, M-pesa, Airtel Money, Maxi malipo au kupitia kadi yako ya benki (ATM Card za NMB na UMOJA SWITCH). Unatakiwa kulipa faini yako ndani ya siku saba. Baada ya siku saba utatozwa ziada ya 25%, baada ya siku kumi na nne na kuendelea utatozwa ziada ya 50% ya tozo la awali na itakuwa ikiongezeka kadiri unavyochelewa kulipa. Kwa wale watakaokamatwa wakati wa oparesheni watafikishwa mahakamani ambapo mbali na kulipa malimbikizo ya tozo watatozwa faini ya TZS 50,000/= au kifungo cha miezi miwili jela.
Ndugu Wanahabari,
Ili kulipia kwa njia ya mitandao ya simu namba maalum ya Polisi (USSD Code) itakayotumika ni *152*75#. Namba hii pamoja na kutumika katika kulipia tozo pia unaweza kuangalia iwapo gari lako linadaiwa tozo la notification lililolimbikizwa.
Ndugu Wanahabari,
Baada ya kutolewa tiketi hiyo dereva husika atatakiwa kulipa faini yake kwa njia hizo zilizotajwa kisha kuiwasiliha kwa askari mwenye mashine namba ya kumbukumbu ya malipo aliyoipata kupitia mtandao husika. Namba hiyo ya kumbukumbu itaingizwa kwenye mashine ya kutolea tiketi ambapo itatolewa risiti ya malipo kisha kukabidhiwa kwa dereva husika.
Ieleweke kwamba, ulipaji huu wa tozo kielektroniki hauna tofauti na ule unaotumika katika kulipia umeme wa LUKU au ada za Magari zinazotozwa kwa njia ya mtandao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Ndugu Wanahabari,
Ili kurahisisha zoezi hili la ulipaji faini kwa njia ya kielektroniki, madereva watatakiwa kutembea na leseni zao halisi za udereva vinginevyo watalazimika kupelekwa vituoni kwa ajili ya kupata taarifa zao za leseni kutoka katika computer za mfumo wa leseni za udereva jambo ambalo linaweza kuwapotezea muda.
Aidha ieleweke kwamba dereva anapoandikiwa faini ya kielekroniki akichelewa kulipa katika muda aliopewa, Jeshi la Polisi litakuwa likiendesha oparesheni mara kwa mara kwa kuyamulika magari yote yanayodaiwa faini kwa kutumia mtambo maalum wa kutambua namba za usajili wa magari yanayodaiwa (Automatic Number Plate Recognition System). Watakaokamatwa katika oparesheni hizi kwa kukwepa kulipa faini, mbali na kutakiwa kulipa faini aliyolimbikiza awali pia atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sharia.
2. KANUNI YA KUWEKA NUKTA KATIKA LESENI ZA UDEREVA
Ndugu wanahabari,
Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168 kama ilivyorejewa mwaka 2002, Kifungu cha 25A na 114(h) imeweka Kanuni ya uwekaji nukta katika leseni za udereva (THE ROAD TRAFFIC (DRIVERS LICENSE POINT SYSTEM).
Mfumo wa ulipaji faini kwa njia ya kielektoniki utakwenda sambamba na Kanuni ya uwekaji wa nukta katika leseni za udereva kulingana na uzito wa kosa lililotendwa na dereva.
Mfano, dereva akishtakiwa kwa kosa kutofunga mkanda wa usalama atapata nukta 1, akishtakiwa kwa kosa la uendeshaji wa hatari atapata nukta 3, akishtakiwa kwa kosa la mwendokasi atapata nukta 5. Nukta hizi zitakapotimia 15 leseni ya dereva husika itafungiwa kwa kipindi cha miezi sita.
Ndugu wanahabari,
Ndugu wanahabari,
Mwisho nitoe wito kwa madereva na wananchi kwa ujumla kutupa ushirikiano katika kutekeleza mfumo huu mpya wa ulipaji wa faini za papo kwa hapo katika Jiji la Dar es salaam na hatimaye tutakapoanza nchi nzima.
ENDESHA SALAMA – OKOA MAISHA.
Imetolewa na:
MOHAMMED R.MPINGA – DCP,
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)
No Comment! Be the first one.