Leo lile balaa linalowakuta watu wenye majukumu ya kusimamia akaunti za makampuni ya utengenezaji simu au ata mara nyingine watu mashuhuri wenye majukumu ya kutangaza bidhaa za simu (Ambassadors) limewakuta Huawei Tanzania kupitia akaunti yao ya Twitter.
Msimamiaji wa akaunti hiyo ametuma ujumbe kama Huawei Tanzania huku akitumia simu ya iPhone kujisahau ya kuwa mwishoni Twitter wangeandika ni simu ya aina gani ujumbe huo umepitia!!!!! Tazama picha, ila inaonekana wamefanya mabadiliko mara moja kwa kufuta na kutwit upya.
Kosa hilo liligunduliwa na mtumiaji wa Twitter mmoja, ndugu Bernard Chuma naye akatwit kama hivi;
Huawei Device but mnatumia iPhone!
No Comment! Be the first one.