Maboresho ya programu tumishi mbalimbali kila siku yamekuwa yakishika chati, yote ni kuzidi kuwapa raha watumiaji wake huku ikizidi kutaka kujizolea watu wengine zaidi.
WhatsApp sasa wameamua kuja na sasisho jipya ambalo litawapa nguvu zaidi wamiliki/viongozi wa makundi kwenye WhatsApp kuweza kuamua kutuma ujumbe wao pekee ambapo watu wengine ambao watakuepo ndani ya kundi watashindwa kutuma ujumbe au kujibu kama ilivyo kawaida.
Uwezo huo mpya umejikita katika kuifanya zaidi WhatsApp kuwa mojawapo ya chombo cha kusambaza taarifa na pia kudhibiti baadhi ya mitafaruku kadhaa ambayo inaweza kujitokeza ndani ya kundi.
Kutoka sasisho lililopita, WhatsApp kwa sasa imeruhusu kuweka maelezo kidogo kuhusu kundi; linahusu nini na pia kuweka uwezo wa kufunga/kuruhusu watu gani waweze kubadirisha jina la kundi pamoja na picha. BOFYA HAPA kujua zaidi.
Uwezo huu kwa sasa upo katika toleo la majaribio la WhatsApp Beta pamoja na baadhi ya simu za Windows pia iOS wameanza kufurahia huduma hiyo, huku sio muda huduma hiyo inatazamiwa kusambazwa kwa watumiaji wote duniani kote.