Sasa ni rasmi kwa wanaotaka Visa kwenda Marekani maombi yao yatahusisha kuorodhesha akaunti zao za mitandao ya kijamii.
Katika jambo la ajabu ni kwamba taarifa zitakazohitajika hazitakuwa za siku au muda huo bali watahitaji pia anuani za barua pepe na namba za simu ambazo umeshawahi kumiliki katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa wenye uhitaji wa kufanya safari za kwenda Marekani kwa sasa itawabidi wajitathimini kwa undani na mambo wanayofanya au kusema kwenye mitandao ya kijamii. Ingawa Marekani ni taifa linaloheshimu sana uhuru wa maoni ila haitashangaza kama tweet au post moja ya mitandao ya kijamii uliyoongea dhidi ya Marekani kusababisha mtu mmoja anayehakiki data hizo kuamua kukunyima VISA.

Historia: Visa ilianza kutumiza zaidi baada ya vitaa kuu vya kwanza vya dunia, ujio wa treni ulihakikisha watu wengi waliaanza kusafiri zaidi kati ya nchi moja hadi nyingine. Utoaji wa VISA huwa unafanyika kwa njia kadhaa: kuna njia ya kugongwa muhuri katika leseni ya kusafiria (passport), ugawaji wa karatasi au kitambulisho spesheli.
Je ni kwa kila aina ya mtu na kwa kila aina ya safari?
Ni watu walio kwenye kazi za kidoplomasia na baadhi ya watumishi wa serikali wanaosafiri kikazi ndio wataweza kunusurika na hitaji hili.
Kwa nini sasa hivi?
Inaonekana Marekani wanachukua hatua nyingi zaidi za kuhakikisha wanachuja sana suala la watu kuingia nchini mwao. Utaratibu huu sio mpya ila zamani ulikuwa ni hitaji kwa watu wanaotoka kwenye mataifa yenye ugaidi tuu.