Kifaa hiki – Vision Pro– kilishatambulishwa kabisa na kampuni ya Apple na kuna baadhi ya watu waliochaguliwa walikijaribu kabisa kifaa hiki.
Vision Pro ilitangazwa rasmi mwezi wa sita na kisha kifaa hichi kikatangazwa kabisa kwamba kitaanza kupatikana katika masoko mwanzoni wa mwaka 2024 – yaani januari
Kwa sasa kampuni ya Apple imeweka wazi kabisa kwamba kipindi hicho kimesogezwa mbele na ujio wake utakua ni mwezi wa tatu ya mwaka 2024.
Apple wenyewe wanasema muda umesogezwa mbele kwa makusudi kabisa maana wanajipanga vizuri zaidi na shughuli zote za usambazaji wa kifaa hicho.
Ukiachana na hilo Apple bado wanakifanyia majaribio kwa zaidi kifaa hicho katika kuhakikisha kabisa kwamba kinafaa kabisa katika soko.
Kumbuka uzalishawaji wa kifaa hichi ni mdogo sana kutoka na mali ghafi na teknolojia yake ambayo inatumika.
Inasemekana kwa kuanzia Apple itaingiza sokoni vifaa hivyo 400,000 tuu kwa kuanzia na itaanzia katika soko la marekani na kisha vitaanza kusambaa katika masoko mengine.
Baadhi ya wafanya kazi wa maduka ya Apple inaonekana wameitwa katika makao makuu (HQ) ya kampuni hiyo na lengo likiwa ni kuwapa matunzo ya kifaa hicho cha Vision Pro.
Vison Pro itakua inaendeshwa na VisionOS ambayo ndio programu endeshi ya mfumo mzima wa kifaa hicho
Ningependa kusikia kutoka kwako je kifaa hiki unatamani kukimiliki au simu za kampuni hiyo zinakutosha? Niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.