Licha ya kuwa wawili hawa ni wapinzani/washindani wakubwa sana ni mara chache sana tumekua tukisikia WhatsApp kumsema Telegram au kinyume chake.
Mengi yameshawahi kutokea na kila mmoja mara nyingi alikua akisemea upande wake bila kusema upande wa mwenzie, lakini hali imebadilika na sasa WhatsApp imesema kuwa telegram kuna baadhi ya vitu anapotosha watu.
Kitu kikubwa ambacho WhatsApp wameishutumu Telegram ni eneo lao la ulinzi na usalama haswa katika taarifa za watumiaji wake.
Ni wazi kwamba mara kwa mara tumekua tukisikia kwamba Telegram ina ulinzi wa hali ya juu na hata kampuni hilo mara nyingi limekua likijinadi hivyo.
Shutuma hazikuishia hapo tuu zimeenda mbali sana, kumbuka mtandao wa Telegram makao yake makuu yako katika nchi ya Urusi…
Shutuma WhatsApp wanazipeleka mbali zaidi mpaka kusema kuwa serikali ya urusi inatumia mtandao huo kama sehemu ya kupata taarifa za siri za watu mbalimbali.
Makampuni mengi ya teknolojia mara kwa mara yamekua yakikubwa na kasumba hii ya kushirikiana na serikali katika kutoa taarifa za watu hata kampuni ya Huawei ilipata shutuma za aina hii.
Wao WhatsApp wanasema kwamba Telegram haina huduma ya End-To-End-Encyption kama chaguo-msingi (default) na utaweza kupata huduma hii katika mtandao huo endapo utaenda na kuanzisha maongezi ya siri (secret chats).
Jambo ambalo katika mtandao wa WhatsApp haliko kama ilivyo kwa mtandao huo pinzani, kingie bado kampuni imekandamizwa maana wamesemekana hata katika huduma za makundi (group) hawana teknolojia hiyo ya End-To-End-Encryption.
Wao Telegram mpaka sasa wanawalaumu WhatsApp kwa kutumia kigezo cha End-To-End-Encryption kama sababu, wanachohisi wao ni kwamba kampuni hiyo imeamua kuwatafutia sababu tuu.
Kingine ni kwamba Telegram wamejitetea kwamba kama mtu anaetumia WhatsApp atafanya backup ya meseji zake katika mitandao kama vile Google Drive basi ni lazima hata…..
…. Google wenyewe watakua na uwezo wa kuona hizo meseji hivyo basi hata serekali yeyote inaweza ikaomba kwa google pengine na ikapewa taarifa hizo sio?
Mtanange ni mkali wewe uko upande upi? Niandikie hapo chini katika eneo la comment? Je unadhani kwa WhatsApp ni mbwembwe tuu au kadhamiria?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.