Vivo ni moja kati ya kampuni kubwa sana ya kutengeneza na kuuza simu na kwa sasa wana mpango wa kuingia katika soko kwa mara nyingine tena kwa mali mpya.
Simu janja za kujikunya (Flip) zinakuja kwa kasi sana na makampuni mengi ya simu ya mpango mkakati wa kutengeneza na kuuza simu hizi na Vivo ikiwa ni moja wapo.
Katika soko la simu za kujikunja linazidi kukuwa sana na soko hili linaongozwa na kampuni ya Samsung ambao wanapata mauzo mengi kuliko kampuni nyingine katika simu janja za aina hii.
Kampuni hili kwa sasa wana simu mbili za kujikunja katika soko ambazo zinajulikana kama Vivo X Fold 2 na Vivo X Flip.
Kampuni bado haijaishia hapo, bado ina mpango wa kauchia simu zingine mbili ambazo ziko katika mfumo wa kujikunja na zitaitwa Vivo S Flip na Vivo V Flip.
Hili limekuja kufahamika mara tuu ya baada ya kampuni hiyo kuhifadhi haki miliki za simu hizo mpya katika bodi zenye mamlaka hayo
Taarifa za undani kabisa kuhusiana na hizi simu hazijawekwa wazi kabisa na kwa sasa linalojulikana tuu ni kwamba simu hizi ni za kujikunja tuu.
Kumbuka simu zingine za kujikunja kutoka Vivo ni kwamba zilikua zinauzika kw asana huko katika soko la china pekee na ni wazi kabisa kwamba hizi mpya zinaweza zikaenda mbali Zaidi.
Ni wazi kwamba tutazidi kupata taarifa kadha wa kadha kuhusiana na simu hizi maana kwa sasa hata sifa za undani hazijatolewa, hivyo tusubirie tamko rasmi.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.