Mtandao wa simu wa Vodacom umeandaa tukio jingine la mauzo makubwa ya simu, tableti na vitu vingine vya elektroniki hapo kesho (Jumamosi).
“Njoo ujipatie simu kali kali kwa bei ya punguzo la hadi asilimia 75%. Hii siyo ya kukosa! Mwambie mwengine amwambie na mwengine na wote tukutane Jumamosi na Jumapili hii. KIINGILIO….BURE BURE KABISA au tuseme ni uwezo wako wa kufika.”
Kupitia Vodacom EXPO huwa wanauza vitu vingi kwa bei nafuu zaidi ukilinganisha na bei za kawaida na wengi huwa wanachukulia hatua hii kama moja ya jinsi ya wao kuanza upya, yaani kutoa kila walichonacho kabla ya kuagiza vifaa (simu, tableti n.k) mpya kila baada ya muda flani.
Kwenye ukurasa wao wa Facebook wa tukio hilo la Vodacom EXPO, wamesema “Njoo ujipatie simu kali kali kwa bei ya punguzo la hadi asilimia 75%. Hii siyo ya kukosa! Mwambie mwengine amwambie na mwengine na wote tukutane Jumamosi na Jumapili hii. KIINGILIO….BURE BURE KABISA au tuseme ni uwezo wako wa kufika.”
Timu yetu ya TeknoKona itaenda maeneo hayo na tutakuambia baadhi ya simu kali zaidi tutakazoziona. Kama upo jijini Dar es Salaam na ulikuwa unafikiria kununua simu hivi karibuni tunakushauri utembelee pia, kwani unaweza kujikuta ukapata simu nzuri kwa bei nzuri sana.
Chanzo | https://www.facebook.com/events/455535367947604/
No Comment! Be the first one.