Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi, Vodacom Tanzania imetangaza mfumo mpya kielektroniki wa usajili kwa wateja wapya.
Mfumo huo mpya utafupisha muda wa usajili wa laini kwa mteja mpya na kumuwezesha kutumia namba zao mpya ndani ya saa moja kutoka muda wa usajili akiwa popote Tanzania. Hii itapunguza adha iliyokuwepo ya kusubiria hadi siku kumi na tano baada ya usajili kutegemea na mahali mteja alipo nchini, ambayo ulihusu kurudisha fomu za usajili makao makuu Dar es Salaam.

Katika mchakato wa usajili huu mpya, mteja ataweza kujisajili kwa wakala wowote maalum wa Vodacom ambapo, wakala atahakiki taarifa za mteja, atapiga picha ya kitambulisho chake na kisha kutuma yote hayo mtandaoni. Baada ya hapo usajili huo utakamilika kwa kutumia namba maalum.
Vodacom inatumaini mfumo huu utamrahisishia mteja kujiunga na mtandao wao na kumuwezesha kufurahia huduma zake bila usmbufu. Mfumo huu unaenda sambaba na sheria za nchi za udhibiti na usalama wa mtandao. Kampuni hiyo inaendelea kuhimiza umma kushiriki katika zoezi la kusajili namba zao za simu na kutoa taarifa za uhakika ili kudhibiti uhalifu na pia kuweza kuwasaidia pindi wapotezapo kadi ya simu na huduma ya M-Pesa.
No Comment! Be the first one.