Ushindani wa makampuni ya simu unazidi kuonekana na kuwa faida kwa watumiaji wa huduma hizo na sasa kwa wale watumiaji wa simu za Blackberry wanazidi kuwa na ‘choice’/uchaguzi mkubwa zaidi baada ya kampuni ya Vodacom nayo kushusha bei ya gharama za malipo ya kabla kwa ajili BIS (Blackberry Internet Service) ambayo huwa inawawezesha wateja kutumia huduma nyingi zaidi za intaneti kwenye simu za Blackberry.
Baada ya Airtel kupunguza gharama za huduma za intaneti kwa Blackberry hapo Juni 1, kampuni nyingine nayo yafanya hivyo.
Kampuni ya Vodacom imeshusha kutoka Tsh 30,000 kwa mwezi hadi Tsh 20,000/= ambayo ni sawa na ile inayotozwa na kampuni ya Tigo. Na ile ya kwa wiki nao wameweka Tsh 7,000/= ambayo ni sawa na ya kampuni ya Tigo.
Hadi kwa sasa Tigo na Vodacom ndiyo wanaotoza kwa bei ya chini zaidi kwa mwezi, kwani tovuti ya Airtel inaonesha wanatoza Tsh 35,000/= (nimejaribu kupata uhakika zaidi kutoka kwao kupitia ukurasa wao wa Facebook na twitter lakini hadi naweka makala hii sijapata majibu yao). Wakati tovuti ya Zantel ikionesha wanatoza Tsh 30,000/= kwa mwezi kwa huduma ya mwezi mmoja.
Kwa upande ya huduma ya wiki Airtel wanabakia kuwa bei rahisi zaidi kwani wanatoza Tsh 5,000/= kwa wiki ukilinganisha na Tigo na Vodacom ambao wote wanatoza Tsh 7,000/= huku tovuti ya Zantel ikionesha wanatoza Tsh 12,000/=.
Kupata huduma za intaneti kwa ajili ya Blackberry yako kupitia Vodacom piga *149*01# na fuata maelekezo!
No Comment! Be the first one.