Bilioni 30 ndani ya siku 100!!!! Yaani zaidi ya Milioni 3.33 kila siku! Moja kati ya mtandao mikubwa zaidi Tanzania wa simu wa Vodacom wamekuja na promosheni inayoweza kupewa sifa ya kuwa kubwa kuliko zote katika historia ya michezo ya bahati nasibu nchini Tanzania ambapo wateja watajishindia pesa taslimu Sh. bilioni 30/- katika zawadi ndani ya kipindi cha siku 100.
Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Rene Meza , “kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”
Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi mia moja wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/- kila siku.
Meza ameongeza kuwa hii inadhihirisha dhamira ya kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi “ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom kila siku.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema ili kushiriki katika promosheni hii, mteja yeyote wa Vodacom, aliyeko popote nchini anahitaji kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY”. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.
“Tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions ni rahisi sana kushiriki. Tuma ujumbe mfupi mmoja tu na mara moja tu kila siku. Hakuna maswali mengi, wala chemsha bongo na hivyo kufanya hii kuwa promosheni inayotoa nafasi kwa wateja wengi kuibuka washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku unatuma ujumbe mfupi,” Twissa.
Kwa muda mrefu hapajakuwa na promosheni kubwa ya kugawa pesa kwa wingi kutoka kampuni za simu, kampeni ya mwisho kubwa ya zawadi ilikuwa ni ya nyumba 3 kutoka mtandao wa Airtel iliyotambulishwa mwaka 2013.
Kwa kiasi kikubwa kulingana na kiwango cha zawadi na njia rahisi ya ushiriki (kwa gharama ya Tsh 300 tuu) si vibaya kusema promosheni hii inaweza kufanikiwa sana, lakini pia TeknoKona tunategemea kampuni zingine kama vile Tigo na Airtel zinaweza kuja na promosheni zao muda wowote kuanzia sasa kujaribu kuizima hii au kufurahisha wateja wao pia. Muda utaongea!
No Comment! Be the first one.