Utengenezaji wa magari yanayotumia nishati ya umeme ni teknolojia ambayo imeonekana kuwa rafiki na mazingira hivyo kufanya kampuni nyingi tu kutengeneza magari ambayo yanaendeshwa kwa umeme na si mafuta (petroli/dezeli).
Volkswagen (VW) imeamua kuwekeza katika magari yanayotumia nishati ya umeme badala ya kuendelea utenenezaji wa magari yanayotumia nishati ya mafuta. VW imepanga kufikia mwaka 2025 kuwa na matoleo 80 tofauti tofauti ya magari yanayotumia nishati ya umeme.
Chanzo cha nishati ya magari yanayotarajia kutumia nishati ya umeme kutoka VW.
Katika utekelezaji wa adhma hiyo kutoka VW itatumia madini ya Cobalt katika utengnenezaji wa betri zenye uwezo wa kuongezwa nguvu (kuchajiwa) baada ya muda fulani ambapo betri hizo ndizo zitakuwa zinaendesha mfumo mzima wa gari.
Jamhuri Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ni moja ya nchi zinazozalisha kwa wingi madini ya Cobalt na tayari VW wameshaingia makubaliano na DRC kuweza kununua madini hayo ingawa VW wamesema watahakikisha kuwa upatikanaji wa madini hayo hautatokana na kutumikisha watoto wadogo.
Betri zinazotumika kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme yanatumia madini ya Cobalt pamoja na mchanganiko wa madini ya chuma na Nickel jambo linaloongeza ufanisi wa magari hayo na kuwa na dhamana ya kati miaka 8-10.

Volkswagen yenye makao yake makuu huko nchini Ujerumani itakumbukwa na wengi kuwa kampuni hiyo ilishawahi kuingia katika sakata la udanganyifu kwenye magari yake jambo lililoisababishia kampuni hiyo hasara ya mabilioni ya dola hata kutoza iaminifu kutoka wapenzi wa Volkswagen.
DRC ndio nchi inayozalisha kwa wingi duniani kote madini ya Cobalt (65% ya madini ya Cobalt yanatoka DRC). Nchi nyingine ni pamoja na Urusi, Uchina, Canada, Zambia na Australia.
VW haitegemei kujihusisha na udanganyifu wa aina yoyote ile bali imejipanga kuleta ushindani mkubwa wa kampuni kama Tesla, Google na nyinginezo ambazo zinazojihusisha na utengenezaji wa magari yanayotumia umeme.
Vyanzo: Reuters, Fortune