Niantic ni kampuni yenye jina kubwa katika ulimwengu wa magemu na mpaka sasa inatamba sana na gemu lake la Pokemon GO.
Waandaaji hao wa gemu la Pokemon GO wametangazwa kwamba wataachisha kazi wafanyakazi 230 hii ikiwa ni namba kubwa sana kwa wakati mmoja.
Kampuni pia imeeleza kusikitishwa kwako na uamuzi huo japo sio hivyo tuu kampuni pia itaacha kuzalisha baadhi ya magemu ikiwemo Marvel: World of Heroes.
Lingine ambalo limewashtua watu wengi ni kwamba kampuni vile vile inafunga moja ya studio zake kubwa iliyopo katika jiji la Los Angeles.
Na vile vile wanaachana na gemu la NBA All-World, hatua hizi zote zimeonekana zikiwaumiza sana mashabiki na hata baadhi ya wafanyakazi wa kampui hiyo.
Wakuu wa kampuni wanasema kampuni ilikua kwa kiasi kikubwa na kwa haraka sana wakati wa kipingi cha gonjwa la CORONA (Uviko 19) ambapo kampuni ilikuwa kwa ukubwa sana kulingana na mazingira yale
Kwa sasa mazingira yamebadilika na hivyo basi kampuni haina budi kuweza kuendana na mazingira mapya jinsi yanavyotaka.
Kingine ni kwamba kampuni bado haipati mapato makubwa kama vile ilivyokua inapata mwanzo wakati mambo yalipo kuwa mazuri zaidi.
Niantic ni moja katika ya makampuni ya magemu ya kwanza kwanza kabisa kupata umaarufu mkubwa kwa kutumia teknolojia ya AR (Augmented Reality)
Kampuni imewaka wazi dhamira yake ya kutaka kuendelea kuiliboresha gemu hilo la Pokemon GO maana bado lina uhitaji mkubwa sana
Kingine ni kwamba katika tasnia ya teknolojia kwa mwaka 2023 mpaka sasa ni kwamba kuna jumla ya wafanya kazi zaidi ya 211,630 ambao wameshaachishwa kazi na hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Layoffs.fyi
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani kampuni hii itarudi na kuanza kufanya vizuri kama zamani?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.