Waanzilishi wa Instagram, Kevin Systrom na Mike Krieger wametangaza kuwa wanaondoka katika kampuni hiyo na kwenda kujaribu udadisi na ubunifu wao sehemu nyingine.
Bw. Kevin Systrom kabla ya kutangaza kuondoka ndiyo aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Instagram. Instagram ambayo ilinunuliwa na Facebook mwaka 2012 kwa dola bilioni moja taslim ambapo kwa sasa ina watumiaji zaidi ya bilioni moja duniani kote.
Hatua ya kuondoka kwao inatokea huku kukiwa na taarifa za mvutano kati ya waasisi hao wa Instagram na uongozi wa Facebook ambayo ni kampuni mama. Hatua hiyo ni kama pigo kwa Facebook baada ya waanzilishi wa WhatsApp nao kujiweka pembenimiezi kadhaa iliyopita.