Wadukuzi walipwa takribani Tsh Bilioni 200. Katika tukio la kihistoria, kampuni ya Cencora, imelipa dola milioni 75 kupitia mfumo wa malipo ya Bitcoin baada ya kushambuliwa na kundi la wahalifu wa mtandao linalojulikana kama Dark Angels. Haya ni malipo makubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya uhalifu wa mtandao.
Shambulio hili lilianza mwezi Februari 2024, wakati Cencora ilipogundua uvunjaji wa data kwenye mifumo yake. Wahalifu walidai malipo ya dola milioni 150, lakini baada ya mazungumzo, kiasi hicho kilipunguzwa hadi dola milioni 75. Malipo yalifanyika kwa awamu tatu mwezi Machi, na jumla ya Bitcoin 1,091.5 zilitumwa kwa wahalifu.
Thamani ya Malipo kwa Shilingi za Kitanzania
Kwa kutumia kiwango cha ubadilishaji wa sasa, ambapo dola moja ya Marekani ni sawa na takriban shilingi za Kitanzania 2,700, malipo haya ya dola milioni 75 yanakadiriwa kuwa sawa na shilingi bilioni 200.
Athari za Shambulio
Shambulio hili limesababisha upotevu wa data muhimu ikiwemo majina, anwani, tarehe za kuzaliwa, na taarifa za matibabu za wateja wa Cencora. Hali hii imeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa sekta ya afya, ambayo imekuwa ikilengwa zaidi na mashambulio ya ransomware kutokana na umuhimu wake na uwezo wa kulipa fidia kubwa.
Ukuaji wa teknolojia na ongezeko la vifaa vya huduma za kijamii ambazo zimeunganishwa na mfumo wa intaneti utazidi kuongeza hatari ya udukuzi. Sekta ya usalama wa kimtandao inategemewa kuzidi kukua kutokana na makampuni mengi kuepuka athari zinazoweza tokea kutokana na kutokuwa na ulinzi dhabiti wa kimtandao.
No Comment! Be the first one.