Saa Janja (Smart Watch) ambazo zinachukua muonekano (design) kama ule wa saa za Apple maarufu kama iWatch zimeanza onekana katika masoko ya kimtandao (online shops) mbalimbali huko nchini china.
Picha za simu za Apple ambazo zinauzwa kwenye masoko hayo hazi jaandikwa neno ‘Apple Watch’ bali tunda la epo limewekwa badala ya neno ‘Apple’ na kufuatiwa na neno ‘watch’.
Kutokana na kwamba iWatch zimetangazwa na kuongelewa sana kwenye mtandao, hali hii imefanya watu wengi na wateja kwa ujumla kujua au kuwa na wazo kuwa itakua na muonekano upi. Mambo yote haya yamewafanya watu kujua jinsi ilivyo ki undani zaidi na vipengele vyake. Hii pia imesaidia watu kuweza kutofautisha saa janja ya Apple katika saa janja zingine
SOMA PIA: iWatch: Apple Na Saa Ya Milioni 18+
Licha Ya Kwamba iWatch inakaribia kuingia sokoni rasmi baadhi ya wafanya biashara wakubwa wamechukulia hii kama ni fursa. Wametoa na kuuza saa zao ambazo ni feki huko china, Ndio kabisaaaaa! Saa hizi ni bei rahisi sana kulinganisha na bei ya saa orijino kutoka Apple
Mfano mzuri ni kwenye soko la kimtandao la kimataifa la Alibaba. Mtandao wa Taobao (www.Taobao.com) ambao umeweka bidhaa kama AW08 na iWatch katika mtandao huo. Badala ya saa hizi kuwa na ‘Apple watch OS’ cha kushangaza Taobao wameweka ‘Apple Watch’ za kwao kwa kuwa zina zinatumia mfumo wa Android wa google

Samahani nipo nje ya maada kidogo naulizia applications itakayo niwezesha kuperuzi website ambazo zipo recommend kwa baadhi ya nchi.
GabrielMathewAlaMgongolo inawezekana soma hapa -> http://teknokona.com/2014/11/26/hola-fungua-mitandao-inayozuiwa-kufunguka-tanzania/