Wanaanga wanne wa Marekani wanapanga kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 Novemba mwaka huu kutoka kwa obiti, wakiendeleza mazoea ya watu kupiga kura zao kutoka angani.
Mwanaanga wa kwanza anayepangwa kufika katika kituo cha anga cha kimataifa kabla ya uchaguzi ni Kate Rubins, ambaye anazindua roketi ya Urusi-Soyuz mnamo Oktoba 14 pamoja na wanaanga wawili wa Urusi. Rubins alikiambia chombo kimoja cha habari kuwa ana mpango wa kumchagua rais akiwa kwenye anga la mbali. “Nadhani ni muhimu sana kwa kila mtu kupiga kura”-Rubins. Ikiwa tunaweza kuifanya kutoka angani, basi naamini watu wanaweza kuifanya kutoka ardhini, pia”, aliongeza Bi. Kate.
Halafu atajiunga na wanaanga wengine watatu wa Marekani-Mike Hopkins, Victor Glover, na Shannon Walker – ambao watakuwa kwenye roketi ya pili ya SpaceX mnamo Oktoba 31, pamoja na mwanaanga wa Kijapani Soichi Noguchi. Pia wanapanga kupiga kura kutoka kwa obiti.
Kutoka kushoto kwenda kulia: Wanaanga wa NASA, Shannon Walker, Victor Glover, na Mike Hopkins. Mwingine ni mwanaanga wa Kijapani, Soichi Noguchi.
NASA ina uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kupeleka wataalamu wa masuala ya anga kabla ya safari wanaanga hujaza fomu ya kueleza kutokuwepo kwao (sawa na ile ambayo wanajeshi wanajaza pale ambapo wanakuwa hawapo). Na mara baada ya fomu hizo kuthibithishwa sanduku la kupiga kura za majaribio hupelekwa NASA katika hali ya usalama.
Baada ya makaratasi ya kupiga kura kufika NASA hujaribu kuona kama inawezekana kuyajaza kwa kutumia kompyuta. Hilo likiwezekana basi NASA huwatumia wanaanga wake makaratasi hayo kwa njia ya barua pepe na wao hupiga kura kisha kurudisha tena kwa NASA na wao kuyatuma kwenye ofisi mbalimbali za kaunti.
Mtumizi ya teknolojia yanavyowezesha mtu kufanya vitu vingi bila ya mhusika kuwepo eneo husika.
Hayo ndio mambo ya teknolojia yanavyoweza kurahisisha vitu sehemu ambazo unaweza kufikiri jambo fulani haliwezekani kumbe vitu vimeshakuwa vyepesi kutekelezeka.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.