Wanawake wamekuwa wakifanya kazi katika sekta mbalimbali hivyo kuleta mchango wa katika ukuaji wa uchumi wa taifa husika na kuwa mojawapo ya nguvu kazi na mtu muhimu kwa maendeleo ya nchi. Je, wanawake kwenye masuala ya teknolojia wapo?
Wanawake ni kundi ambalo wamekuwa wakijichanganya kwenye sekta mbalimbali ambapo huko nyuma kazi za kwenye sekta hizo zilionekana kuwa ni za wanaumw tu lakini miaka kadhaa sasa tumekuwa tukiwapata wanawake wahandisi, madereva na hata wadukuzi pia.
Kwa Tanzania idadi ya wanawake ambao ni wataalamu wa masuala ya teknolojia bado si kubwa ingawa wanathubutu kusoma na kuhitimu masomo ambayo yaaminika kuwa ni magumu na hivyo kuaminika kwamba ni wanaume tu ndio wanayaweza masomo hayo. Makala hii inaangazia wanawake waliopo kwenye sekta ya teknolojia kama heshima ya kuadhimisha siku ya wanawake ulimwenguni.
1. Mrs. Esther Lugoe Mengi (Kutoka Tanzania)
Ni mmoja kati ya watu walionivutia sana kwenye kongamano la TEHAMA mwaka 2017 kwa kile ambacho alikizungumzia kuhusu masuala ya ulinzi kwenye kompyuta, mawasiliano na na masuala ya teknolojia kwa ujumla wake. Mrs. Esther Lugoe ni mtaalamu na aliyebobea masuala ya ulinzi wa kompyuta na akiwa mwazilishi mwenza wa Srensic Africa LTD. Pia, ni mdukuzi anayetambulika (certified hacker). Kuona wasifu wa Esther Lugoe BOFYA HAPA.
2. Judith Owigar (Kutoka Kenya)
Wapo wanawake wengi nchini Kenya ambao wapo kwenye sekta ya teknolojia na TEHAMA kwa ujumla lakini Bi. Judith Owigar amenivutia kutokana na kile ambacho anakifanya. Judith Owigar ni mwazilishi mwenza na rais wa Akirachix kampuni inayotafuta na kuwasaidia wanawake wanajishughulisha na masuala ya teknolojia nchini Kenya.
3. Barbara Birungi Mutabazi (Kutoka Uganda)
Ni mwanamke aliamua kuongeza idadi ya wanawake kwenye sekta ya teknolojia kwa kuanzisha programu aliyoiita “Women in Technology Uganda” mwaka 2012. Programu hii inalenga kuwaelimisha, kuwapa msukumo kwenye masuala ya kompyuta na kuondoa ile kasumba ya kwamba kompyuta ni kazi ya kiume wakati hata wasichana/wanawake wanaweza kuwa wataalamu wa masuala ya kompyuta.
One Comment
Comments are closed.