Suala zima la matangazo mbalimbali kwenye simu janja yamekuwa chanzo cha mapato kwa wahusika lakini sasa wale ambao wanatumia “Njia fupi” kupata huduma ya Spotify ya bure takwimu zao zaongenezeka 🙄 🙄 🙄 .
Watumiaji wanaotumia app ya Spotify kupata huduma ya kusikiliza muziki kwa njia ya intaneti (stream) wamekuwa wakiyakimbia matangazo ambayo yamekuwa yawetumwa kwenye Spotify.
Wateja takribani milioni 2 wa Spotify wanaonekana kuyazuia matangazo hayo. Mpaka kufikia Desemba 31 2017 Spotify ilikuwa na wateja hai 157 milioni na 86 milioni kati yao walikuwa wanalipa kutapta huduma ya Spotify isiyokuwa na matangazo.

Hali hiyo inatishia sana kwani mapato ya Spotify yanashuka kutokana na kitendo hicho ambacho watu hao takribani milioni 2 wanatumia huduma ya kutopata matangazo bila ya hata kulipia. Jambo hilo linaweza kusababisha Spotify kuwekwa katika soko la hisa ili ipate pesa za kuendesha shughuli zake; hii itamaanisha kuwa Spotify itakuwa inamilikiwa na wanahisa.
Je, wewe ni miongoni mwa wale watumiaji milioni 2 wa bure kwenye Spotify? Kampuni hiyo imeonya kusitisha/kuwafuta kabisa watakaobainika kutumia Spotify ya bure kwa njia ambayo haistahili.
Vyanzo: The Verge, NzHerald
One Comment
Comments are closed.