Mtendaji mkuu wa Twitter Jack Dorsey amethibitisha kwa tweet kwamba watendaji muhimu wanne wanaondoka na kuachana na Twitter.
Kevin Weil aliyekuwa mkuu wa bidhaa, Katie Jacobs aliyekuwa mkuu wa habari, Katie Jacobs ambaye alikuwa mkuu wa uhandisi pamoja na Skip Schipper ambaye alihudumu kama mwajiri wanategemea kuondoka na kuachana na Twitter.

Akitangaza uamuzi huo mkurugenzi mtendaji wa Twitter amesema kwamba alitarajia kuongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo baadaye wiki hii lakini kutokana na tetesi za taarifa hiyo analazimika kuweka mambo sawa.
Bosi huyo wa Twitter amewashukuru kwa mchango wao watendaji hao wanaoondoka, akisema kwamba wameweza kufanikisha malengo yao kwa ulimwengu na kwamba watendaji hao ni watu wa kipekee saana.
Kuziba mapengo ya walio ondoka Jack amesema kwamba Adam bain ambaye ni mkuu wa operesheni atashika majukumu yote ya bidhaa zinazohusiana na makusanyo pamoja na timu za habari na zimu za HR, wakati afisa teknolojia Adam messinger atashika timu za uhandisi ubunifu na uchunguzi.
Jack amehakikisha kwamba atafanya kazi bega kwa bega na Messinger ili kuhakikisha wanatengeneza bidhaa zilizobora.

Habari hii ilipoingia mitandaoni iliibua tena tetesi ambazo zilikuwa kama zimesahaulika, moja ya tetesi ni kwamba Twitter itauzwa lakini jambo la msingi kujua hapa ni kwamba mwaka 2015 haukua mwaka mzuri kwa mtandao huu kwani haukuwa na ukuwaji mkubwa wa watumiaji na kama kutonesha kidonda mtandao wa Instagram uliipiku Twitter baada ya kupata watumiaji milioni 400 dhidi ya watumiaji milioni 300 wa Twitter.
Twitter inategemea sana kurudi katika soko kwa kuingiza kipengere chake kipya ambacho bado kipo katika majaribio hukuo Uingereza kinachoitwa Moments ambacho kinatumika kukusanya habari za tukio la ainamoja katika timeline ambazo wakati mwingine zinakuwa zimepoooza.
Ni vizuri ikakumbuka kwamba mwanzoni wengi walikuwa na shaka na mtandao huu kama utaweza kufikia malengo yake kwa sababu ya kutumia herufi 140 tu. Wawekezaji walipata wakati mgumu kuamini kwamba bidhaa hii ingeweza kufanya vizuri sokoni kwa sababu ilikua inatumia herufi chache, lakini Twitter iliweza kuvuka changamoto hiyo hivyo halitakuwa jambo la ajabu kuvuka changamoto hii pia.
No Comment! Be the first one.