Netflix ndio kinara wa huduma za burudani kwa njia ya ku’stream, kampuni ilifanya makadirio ya ongezeko la watumiaji wake lakini hali halisi imekuja kuwaacha mdomo wazi.
Kampuni imeweka wazi ripoti yake ya mwisho (ya nne) kwa mwaka 2022 na inaonyesha ongezeko kubwa la idadi ya watumiaji wa mtandao huo wa Netflix kuongezeka ndani ya kipindi cha muda mchache.
Kama una kumbukumbu nzuri tuliandika kuhusu kampuni kupoteza watumiaji wake >>HAPA<< lakini kwa sasa wameweza kugeuza gurudumu.
Kwa harakaharaka ni kwamba kampuni ilikua inadhani kuwa intaongeza wateja wapatao milini 4.5 tuu lakini cha kushangaza ni kwamba mpaka kipindi cha robo nne ya mwaka inaisha wakawa wamepata zaidi ya watumiaji milioni 7.6.
Kumbuka namba hii yote imepatikana ndani ya kipindi cha miezi minne tuu mpaka mwaka 2022 kuisha lakini kuna sababu kadha wa kadha ambazo zimepelekea jambo hili kufanikiwa
Kwa mfano tangia kampuni kupoteza wateja ilijipanga vyema na kuongeza vipengele vingi katika jukwaa lao mfano waliongeza magemu, kupunguza baadhi gharama za vifurushi na kuleta aina mpya ya vifurushi. Soma zaidi >>HAPA<<
Kuongeza maonesho mbalimbali katika mtandao huo ambayo mengine yamevunja rekodi kadhaa mfano ile tamthilia ya WEDNESDAY n.k
Hii ni sawa kabisa na kusema kwamba mpaka mwaka 2022 kuisha Netflix imekua na jumla ya watumiaji zaidi ya miloni 230 na namba sahihi kabisa ambayo wao wameitaja ni milioni 230.75.
Kabla ya namba hiyo wao walitabiri kumaliza mwaka na watumiaji milioni 227.59 ambapo walishangaa kupata ongezeko kubwa tuu.
Ukiachana na hayo yote ni wazi kabisa katika Nyanja hii, Netflix ni moja kati ya kampuni ambalo linafanya vizuri sana na mara kwa mara wamekua wakiendana na matakwa ya wateja wao katika kuhakikisha kuwa wanajiboresha zaidi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unafikiri kampuni nyingine katika soko hili zinaweza kufikia namba hizo za Netflix?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.