Tokea ujio wa Windows 10, tatizo kubwa limekuwa usalama wa masasisho yake (Updates). Mara kwa mara updates/masasisho yanayotumwa na Microsoft kwa watumiaji wake yamekuwa yakileta matatizo makubwa kwa baadhi ya watumiaji wa kompyuta zinazotumia toleo hilo la Windows.
Na sasa kuna toleo la sasisho jipya ambalo unashauriwa kutokubali liingie kwenye kompyuta yako kwa sasa. Toleo la sasisho linalokwenda kwa jina la Windows 10 2004 limeanza kusababisha matatizo mbalimbali kwenye kompyuta za watu duniani kote. Microsoft na watafiti wengine wanawashauri watumiaji ambao bado hawajadownload sasisho hili kusubiri.

Matatizo yanayotokea kwa baadhi ya kompyuta pale panapokuwa na makosa kwenye masasisho ya Windows ni pamoja na;
- Baadhi ya mafaili kupotea
- Kioo kujaa rangi ya bluu, maarufu kama ‘blue screen’
- Muingiliano baina ya mifumo ya graphic card na hivyo kwa watumiaji hasa wa kompyuta za mezani (desktop) kuona tatizo la ‘No signal’. Monitor/TV kutoweza kuwasiliana na kompyuta kuu.
- Kipanya kutofanya kazi vizuri
- Matatizo kwenye sauti n.k.
Hatua za kuchukua
Kwa sasa ushauri mkuu ambao Microsoft ameutoa ni kuepuka kufanya sasisho lolote, hasa hasa kama utaona limepewa jina la Windows 10 2004. Wanafanyia kazi na labda baada ya wiki au zaidi wataleta sasisho jipya lenye utatuzi wa tatizo la sasa.