Dola bilioni 19 nmi nyingi sana na mpaka kampuni lingine lijitokeze kununua lingine kwa thamani hiyo basi bila shaka hilo kampuni litakua linafanya vizuri. Kampuni ya Western Digital imeweka hadharani kuwa italinunua kampuni la Sandisk
Kampuni la Western Digital ni kampuni ambalo limejikita katika kutengeneza ‘Hard disk’ wakati kampuni la Sandisk ni kampuni ambalo limejikita katika kutengeneza memori kadi na ‘USB Flash Drive’. Pia Sandisk ni kampuni la tatu duniani kwa ukubwa katika yale yanayotengeneza memori kadi.
“Tunataka kuwa na vifaa vya ujazo wa aina mbalimbali katika soko la ujazo duniani. Tunataka kujikita katika kuwa na teknolojia ya juu katika ujazo huo pia tunataka kuwa na jukwaa la kutengeneza vifaa mbalimbali na vya kipekee kwa wateja wetu” – CEO wa Western Digital, Stephen Milligan
Kampuni la Sandisk lilianzishwa mwaka 1988 na lilianza kwa jina la SunDisk baada ya miaaka kadhaa likawa linatambulika dunia nzima. Wakati kampuni la Western Digital limeanzishwa miaka 45 iliyopita na limejikita katika aina mbalimbali za ‘External hard drives’ (hard disk za nje –eksiteno–).
Dili hili linatarajiwa kukamilika katika robo ya kwanza ya mwaka 2016. Kama dili likikamilika basi CEO atabaki kuwa bwana Stephen Milligan yule wa Western Digital Wakati CEO wa SanDisk atabaki kuwa mmoja kati ya bodi ya wakurugenzi (Board of directors)
Dili hili litaifanya kampuni ya Western Digital kuingia katika soko la Memori kadi kwa mara ya kwanza hata hivyo Sandisk wameshuhudia kushuka kwa soko lao hivi karibuni. Kumbuka watu hawanunui memori kadi kwa sana kama zamani siku hizi.
Tungependa kusikia toka kwako, wewe umelipokeaje hili?.. Kwa habari kadha wa kadha kama hizi usisite kutembbelea Www.TeknoKona.Com kila siku. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia
One Comment