Kikawaida huduma ya WhatsApp ilikuwa ni bure mwaka wa kwanza, na kisha takribani dola moja kwa mwaka baada ya hapo. Kuanzia sasa huduma hiyo itakuwa bure bila malipo yeyote.
Mmoja wa wanzilishi wa WhatsApp, bwana Jan Koum amesema hayo jijini Munich jumatatu hii. Huduma ya WhatsApp iliyonunuliwa na Facebook miaka kadhaa iliyopita kwa muda mrefu haijawa inatengeneza faida na hili ni kutokana na msimamo wa Bwana Jan wa kukataa matangazo katika huduma hiyo.
Akiwa katika mkutano unaofahamika kama DLC amesema hawataki watu wapate mawazo ya kwamba siku moja huduma wanayoitegemea watapokonywa kisa tuu wameshindwa kufanya malipo na hasa ukizingatia kuna baadhi ya watumiaji wa huduma hiyo hawana ata akaunti za benki za kimataifa ndani ya mfumo wa VISA au MasterCard.
Baada ya kufanya huduma hii kuwa bure kabisa amesema wataangalia kutengeneza mapato kupitia kutoa huduma hiyo kwa makampuni /biashara ingawa bado hatataka iwe katika mfumo wa kimatangazo. Njia kuu inayoonekana inaweza kutumiwa ni kuwezesha makampuni kuwasiliana na wateja wao kwa urahisi na huduma zingine kama hizo.
Ikiwa chini ya Facebook WhatsApp inauwezo wa kuendelea kufanya kazi bila kutegemea mapato yeyote ila ni muhimu kuanza kufanyia kazi suala la kuweza kutengeneza huduma itakayowezesha kuwaingizia pesa na wengi wanaona wana nafasi kubwa ya kupata mapato kupitia huduma spesheli kwa makampuni. Tayari WhatsApp kupitia blog yao wamesema huduma mbalimbali zinaweza letwa mwaka huu.
“Watu wanashangaa tutaendesha WhatsApp bila malipo na kama taarifa hii inamaanisha ya kwamba tutaanza kuweka matangazo mbalimbali JIBU ni HAPANA. Kuanzia mwaka huu tutafanya majaribio ya huduma mbalimbali zitakazokuwezesha kutumia WhatsApp kuwasiliana na makampuni na mashirika unayotaka kuwa na mawasiliano nayo.
Hii inaweza maanisha kuwasiliana na benki yako kuhusu matatizo au taarifa za akaunti yako, au kuwasiliana na kampuni ya ndege kuhusu safari…… tayari kuna njia zingine kama SMS na kupiga simu zinatumika kwa sasa, ila tutajaribu jinsi ya kurahisisha mawasiliano haya kupitia WhatsApp huku tukifanya hivyo bila kuleta matangazo n.k. “- WHATSAPP
Kama umelipia WhatsApp hivi karibuni fahamu hawatarudisha pesa, na inategemewa taratibu kupitia masasisho (updates) sehemu kuhusu malipo katika app hiyo itaondolewa.
Je una maoni gani juu ya habari hii? Kumbuka kuungana nasi katika mitandao ya kijamii na endelea kusambaza makala kwa ndugu na marafiki.
Chanzo: ReCode
No Comment! Be the first one.