Uwepo wa teknolojia umefanya biashara za watu duniani kuweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi na vitu vikaweza kufanyika bila ya hata kuonana ana kwa ana. WhatsApp Business ni moja kati ya vitu ambavyo vimerahisisha mawasiliano kati ya mfanyabiashara na wateja wake ingawa si kwa wote bali wale wanaoitumia.
Tangu Septemba 2017 kwenye Android mtu anaweza akawa anatumia WhatsApp mbili tofauti; moja ile ambayo wengi tunaifahamu na nyingine ikiwa imetengenezwa ikilenga mambo yanayohusu biashara mathalani kuhusu biashara husika, mahali ofisi ilipo, tovuti/anwani ya barua pepe, n.k.
Tangu wakati huo mpaka Aprili 2019 wanaotumia mfumo endeshi wa iOS nikizillenga simu za iPhone nao sasa wataweza kutumia toleo la WhatsApp mahususi kabisa kwa ajili ya kufanya biashara kidijitali zaidi na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kutenganisha mawasiliano yako na watu wengine na yale yanayohusu biashara pekee.
WhatsApp Business inawezesha mtu kutuma ujumbe wa papo hapo kulingana na alichokiandika, kuweza kuweka ujumbe iwapo umetoka kikazi/utarejea baada ya siku gani.