WhatsApp ni moja kati ya mtandao wa kijamii unarahisisha mazungumzo baina ya watu na vile vile ni moja ya mtandao ambao ni maarufu na una watumiaji wengi sana.
Licha ya kuwa na umaarufu mkubwa mara kwa mara mtandao wa WhatsApp umekua ukija na vipengele kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa unazidi kuwa juu.
Hivi karibuni walikuja na kipengele kipya ambacho kinakwenda kwa jina la Channel na kazi kubwa ya kipengele hiki ni kutuma ujumbe wa njia moja.
Ujumbe huo unaweza kuwa katika mfumo wa maandishi, picha, video, stika na hata maswali katika mfumo wa polls.
Hapa kinafanya kazi kama TV tuu inavyofanya kazi, kwamba taarifa inakua inatoka katika upande mmoja tuu.
Watumiaji ambao wako hai (active users) wa channel hizo za WhatsApp kwa sasa wanazidi milioni 500 kwa mwezi nah ii ni taarifa ambayo imetolewa na mmiliki wa mtandao huo.
Namba hii imefikiwa kwa kipindi cha muda mfupi maana namba hii imekuja baada ya wiki 7 tuu tokea kipengele hiki kianze kutumika WhatsApp.
Bado inaonekana kabisa kwamba WhatsApp itazidi kuja na vipengele vingi vipya na itazidi kuleta maboresho kwa vile ambavyo tayari vipo
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je na wewe ni mtumiaji wa channel?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.