WhatsApp Fingerprint Lock ni kitu kipya ndani ya app ya whatsapp. Kwa sasa watumiaji wa app ya WhatsApp wamepewa uwezo wa kuweka usalama wa kufungua app hiyo kwa kutumia alama za vidole.
Uwezo huo ulianza kusambaa kwa watumiaji wa app hiyo kuanzia jana na usishangae kama bado uwezo huo haujatokea kwako bado, unachotakiwa ni kuhakikisha unatumia toleo jipya kabisa la WhatsApp.

Jinsi ya kuwezesha password katika app ya WhatsApp.
- Fungua app ya WhatsApp
- Nenda eneo la settings – kwa kubofya vidoti vitatu kulia juu kisha bofya ‘settings’
- Bofya ‘Account’
- Nenda kwenye ‘Privacy’
- Shuka hadi chini utaona sehemu imeandikwa ‘Fingerprint lock’.
Hapo utaweza kuwezesesha uwezo huo na pia unaweza kuchagua jinsi unavyotaka app iwe inajifunga.
- Immediately – mara moja baada ya wewe kutoka kwenye app
- After 1 minute – baada ya dakika moja ya kutotumia app hii
- After 30 minutes – baada ya dakika 30
Kama bado eneo hilo halionekani basi rudi kwenye app ya Google Play Store na hakikisha hakuna sasisho (update) la WhatsApp ambalo bado haujadownload. Kama umefanya hivyo na bado basi subiri muda wowote kuanzia sasa uwezo huo utaonekana kwenye app yako.