Unaweza ukawa ukapata ujumbe kama huu: “Unfortunately WhatsApp has stopped”. Saa nyingine hii inatokana na mtumiaji tuu labda unaweza kuta mtumiaji kafungua App ya WhatsApp alafu ghafla akaifunga.
Hata hivyo bado kuna mambo mengi ambayo yanaweza sababusha whatsapp ikawa haifanyi kazi au kuwa na mwendo wa kobe (slow). Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo zinaweza kuiwezesha whatsApp yako kufanya kazi kwa ufasaha kama inavyotakiwa.
FUTA MESEJI
Saa nyingine kitu kinachofanya Whatsapp iwe nzito ni meseji zilizojisevu. Meseji zikiwa nyingi inaladhimu App ya WhatsApp kuchukua muda sana katika mchakato mzima wa kuwahi kufunguka. Jaribu kufuta meseji amabzo sio za muhimu katika App hiyo ili kuacha wazi nafasi amabayo ilikua ina meseji hizo.
ZIMA NA KUWASHA
Kuzima na kuwasha simu pia inachangia kufanya whatsApp na App nyingine (simu kwa ujumla) kutokua ‘slow’, ukizima simu alafu ukaiwasha unaifanya simu kujianzisha apps/programu muhimu tuu hivyo ufanisi wake huongezeka. Inshauriwa kuzima na kuwasha simu yako ingawa mara moja kwa wiki.
Weka Toleo Jipya Zaidi (Update)
Kwa mfumo wa android whatsApp kama haujai ‘Update’ bila shaka haitafanya kazi mpaka ui update. Ujumbe kwama huu utakua unatokea ‘this copy of whatsApp has expired, downlaod to the latest version’ . Fanya mpango na Update whatsApp yako
MEMORI
Lakini labada chanzo ni memori ya simu (RAM), inaweza ikawa unatumia Apps nyingi kwa simu ambayo ina memori ndogo. Hii itakupelekea simu yako kuwa nzito katika kufanya kazi zake. Jinsi ya kuepukana na hili jambo ni kufuta Apps mbalimbali ambazo hazitumiki mara kwa mara na hazina kazi katika simu yako
FUTA KISHA IWEKE UPYA
Kama bado tatizp linaendelea basi futa App hiyo ya WhatsApp kisha iweke tena upya. Jitahidi usirudishe mazungumzo ya mwanzo (back up conversation), hasa kama yalikuwa mengi kwani inaweza ikawa faili ni kubwa sana na linaweza leta tatizo lile lile tena.
Kumbuka mara zote kama imekuwa nzito au haifanyi kazi fuata hatua hizi.
Tembeleza kurasa zatu za Twitter, Facebook na Instagram . comment yako ni muhimu sana
No Comment! Be the first one.