Sio mara ya kwanza mtandao wa kijamii wa WhatsApp kutupa baadhi ya matoleo ya simu ya zamani, kinachofanyika ni kwamba kuna baadhi ya simu/progamu endeshi ambazo WhatsApp inataka kuendana nazo kwa wakati huu.
Orodha imetoka kwa upande wa iPhone na WhatsApp inasema mpaka kufikia mwezi oktoba basi kuna matoleo kadha wa kadha ya iPhone zile za zamani hayataweza kupata huduma ya mtandao huo.
Unaweza ukajiuliza matoleo ya zamani? Hapa kampuni inakua inamaanisha nini—kinachoangaliwa hapa ni program endeshi tuu.
Kwa haraka haraka ni kwamba iPhone zote ambazo zinatumia iOS (program endeshi kwa ajili ya iPhone) 10 na 11 mpaka kufikia mwezi oktoba hazitakuwa na uwezo wa kutumia mtandao wa WhatsApp.
Unaweza ukajiuliza kwanini kampuni inafanya hivi lakini jibu ni dogo sana maana ili kuendana na kasi ya sasa inabidi kampuni ilete teknolojia mpya mpya kwenye App yake ya WhatsApp sio?
Sasa ili hilo liwezekane inabidi vile vile kampuni ihakikishe kwamba katika vifaa ambavyo App yake inatumika, basi vifaa hivyo viwe ni vya kisasa zaidi.
Kumbuka kuna vipengele vingi sana kwa sasa katika mtandoa wa WhatsApp na vingine vipya bado vinakuja na vya zamani vinafanyiwa maboresho vyote hivi vinahitaji vifaa vya kisasa zaidi.
WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo ina nguvu sana kwa sasa na ni moja kati ya mitandao pendwa sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni hizi za kiteknolojia kufanya hivyo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.