Bado mtandao wa WhatsApp unazidi kujisambaza na kuhakikisha kuwa unasambaa zaidi na zaidi, kwa sasa unakuja na App kabisa kwa ajili ya kompyuta za Windows.
Kwa sasa App hiyo inapatikana katika soko la Windows maarufu kama Microsoft store, ifahamike hapo mwanzo watumiaji wa kompyuta walikau wanatumia WhatsApp lakini lile toleo la WhatsApp web.
Pengine watu wanaweza wasione kama hili lina msingi sana sababu huduma ya WhatsApp web ilikuwepo, lakini fikiria hii ni App kabisa ambayo inakaa katika kompyuta yako.
App hii itakua imejiboresha sana katika swala zima la spidi na uaminifu kingine ni kwamba hataka katika upande wa Notification na muundo utakua umeboreshwa sana.
Hii itasaidia sana katika kuhakikisha kuwa mitandao yako yote ya kijamii inapatikana sehemu moja, fikiria kwa watumiaji kama vile makampuni.
Inamaana kwa kutumia kompyuta moja kampuni inaweza ikafanya mambo mengi sana katika kuhakikisha kuwa inajikutanisha moja kwa moja na wateja wake.
Kwa sasa App hii inapatikana katika kompyta zote ambazo zinatumia programu endeshaji ya Windows tuu lakini hata wale wanaotumia MacOS kutoka Apple hawajasahaulika.
App ya WhatsApp kwa program za MacOS kutoka Apple ipo katika majaribio—hii inamaanisha kuwa hivi karibuni tuu na yenyewe itaachiwa rasmi
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje? Je uko tayari kaunza kutumia huduma ya WhatApp kupitia App yake ya Windows?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.