Kipengele hiki ni kizuri sana na kitakua kinafanya kazi kama huduma ya Airdrop au hata Quick Share katika mtandao huo wa WhatsApp.
Kipengele hiki hakitategemea sana kwa watumiaji kuwa na namba ya WhatsApp ya mtu ambae anamtumijia vitu hivyo.
Kipengele hiki kitakua kinafanya kazi baada ya simu hizo kusogeleana kwa ukaribu zaidi na kitafanya kazi kwa kutingisha (shake) simu hizo.
Ndio kutingisha (shake) simu hizo zikiwa karibu ndio itakua uwezo wa kuwasha kipengele hiki na kuanza kurushiana mafaili.
Kingine kizuri ni kwamba mfumo huu utakua bado unatumia teknolojia ya end-to-end encryption kwa maana ya kwanza hakuna upande wa tatu ambao utaweza ona mafaili ambayo yanatumwa kupitia njia hii.
Ni wazi kwanza kipengele hiki kitawezeka kwa watu walio karibu tuu (People nearby) na baada ya kuitingisha simu (shake) mtu wa karibu ataona ombi la kuweza ku’share mafaili.
Kwa sasa kipengele hiki kiko katika hatua za mwanzo kabisa katika uandaaji wake na kinategemewa baadae kuanza kufanyiwa majaribio.
Kipengele hiki kikitolewa kitakua ni moja kati ya mapinduzi makubwa sana kufanyika katika mtandao huo.
Ni wazi kwamba kinasubiriwa kwa hamu, niandikie hapo chini katika uwanja wa coment, je unahisi kiepengele hiki kitakua na watumiaji wengi? Au wengi watatumia njia ya kawaida ya WhatsApp ya kutumiana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.