WhatsApp ni miongoni mwa mitandao ya kijamii ya kuwasiliana na watu ambayo ina watumiaji wengi sana na wengi wakiwa wanakubali ubora/uzuri wa huduma zake.
WhatsApp mara kwa mara imekua ikitoa vipengele kadha wa kadha amabavyo kwa namna moja au nyingine vinafanya mtandao huo kuzidi kuwa juu ukilinganisha na mingine mingi.
Kama hawatafanya sasisho (update) basi watatambulisha vipengele vingine kabisa ambavyo mara ya kwanza havikuwepo.
Kupitia WABetaInfo, taarifa zimewekwa wazi kwani kuna toleo la majaribio ambalo ni namba 2.23.16.19 ambalo linatambulisha kipengele kipya cha Voice Chat katika makundi ya WhatsApp.
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa na kipengele cha Voice Note na kimejikita zaidi katika katika kuhakikisha wana kikundi wanafanya mazungumzo kwa kutumia sauti zao.
Katika mazungumzo hayo ni kwamba yatakua yanafanyika kwa kundi ambalo lina watu zaidi ya 32 lakini ni kwamba wanakikundi mpaka 32 tuu ndio wataweza kushiriki mazungumzo hayo.
Voice Chat hizo zitaweza kuisha baada ya dakika 60 na hii ni kama mwatu watakua hawajajiunga katika mazungumzo hayo.
Uzuri wa kipengele hiki ni kwamba inaruhusu watu kuingia katika mazungumzo ya sauti bila ya simu kuita wala kutoa taarifa (notification) —kwa haraka haraka ni kwamba kuna ukimya wa hali ya juu kwa simu husika
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment hapo chini je unadhani kipengele hichi kitapata watumiaji wengi zaidi kama vipengele vyake vingine kama vile Voice Note?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.