WhatsApp ni moja katika ya mitandao ya kijmaii ambayo ina watumiaji wengi sana ukilinganisha na mitandao mingine mingi.
Licha ya kujipatia jina kubwa sana, bado mtandao huo unaendelea kuhakikisha kuwa unazidi kuleta vipengele kadha wa kadha ambavyo kwa namna moja au nyingine vitafanya mtandao huo kubaki kuwa juu.
Hivi katibuni mtandao wa WhatsApp ulitangaza kuwa utaleta link za kujiunga katika simu za vikundi na familia na kwa sasa kampuni imeshaleta kipengele hicho na vingine kwa watumiaji wa iOS.
Katika toleo hili ni kwamba wakuu wa makundi walikua na uwezo wa kufuta meseji ya mtu mmoja katika kundi na ujumbe huo usionekane na mtu yeyote lakini pia watu watajua ni mtu gani ambae amefuta.
Na kingine ni kwamba kwa wale ambao wanataka kuchomoka/kutoka katika kundi kimya kimya (kwa siri) wataweza fanya hivyo lakini ni kwamba wakuu wa makundi watapata taarif ahiyo.
Kipengele hiki ni muendelezo tuu wa kile kipengele cha kutoka katika kundi kimya kimya bila ya watumiaji wengine kujua chochote.
Kingine ni kwamba toleo hili jipya limekuja na uwezo wa kuwa na Reaction katika eneo la status. Reactions hizo zinakua katika mfumo wa emoji yaaani utaweza kujibu status ya mtu kwa kutumia emoji – haina tofauti na reaction kwa upande wa meseji — kwa haraka zaidi.
Kingine ni kwamba kama mtumiaji ana toleo hili jipya kabisa ni kwamba katika kile kipengele cha “Delete For Me” ambacho mara nyingi huwa watu wanakikosea, sasa unaweza ukakitengua kwa muda kidogo.
Kama kwa watumiji wa Android bado havijawafikia vipengele hizi basi hakuna budi kusubiri….
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je ni kipengele gani ambacho kimekuvutia zaidi katika hivi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.