Mtandao wa WhatsApp unahakikisha kuwa unawapa watumiaji wake aina nyingi za kuwasiliana ukiachana na kutuma ujumbe wa maandishi tuu.
Njia zipo nyingi tuu kama vile kutuma picha,sauti, kupiga simu za sauti au zile za video na kwa sasa WhatsApp wana mpango na kuja na kipengele kingine ambacho kitahusisha kutumiana video fupi fupi.
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kile cha Telegram kwa maana kwamba kitakua kinafanya kazi sawa tuu.
Huduma hii bado haijaanza kupatikana kwa watu lakini chanzo cha kuaminika cha WABetaInfo tayari kimethibitisha hili na watu wako mkao wa kusubiria kipengele hiki.
Kingine cha kuzingatia ni kwamba kipengele hiki kitaanza kupatikana kwa watumiaji wa iPhone tuu na pengine kitaanza kuwafikia watumiaji wa Android kadri muda utakavyozidi kwenda.
Katika kipengele hiki ikumbukwe kuwa kutuma video hizo fupi fupi itakua ni rahisi sana yaani kama vile unavyotuma jumbe za sauti tuu.
kingine ni kwamba video hizi unaweza ukazirekodi mpaka kufikia sekunde 6o tuu, kingine kizuri ni kwamba hutakua na uwezo wa kuzihifadhi (Save) au kuzirusha kwa mwingine (forward) lakini unaweza kuchukua screenshot.
Hili ni jambo zuri ingawa mpaka sasa haijulikani ni lini WhatsApp watafanya kipengele hiki kipatikane kwa kila mtumiaji wa App hiyo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kwa vipengele ambavyo WhatsApp inazidi kuviongeza je itakuja kupata mshindani kweli?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.