WhatsApp ni mtandao wa kijamii ambao umewafikia watu wengi sana na imekua ni msaada mkubwa sana kwa wale wanaotumia simu janja katika mawasiliano.
Mara kwa mara WhatsApp wamekua wakitoa masasisho mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wateja/watumiaji wake wanapata kile kilicho bora kutoka kwao.
Nadhani mara kwa mara umeshwahi sikia kwamba ukituma picha katika mtandao wa WhatsApp huwa picha hizo zinapoteza ubora wake.
Hii ni sawa kabisa kwa maana kwamba kama kuna picha moja itakua inasambaa sana katika mtandao huo ni wazi kwamba kuna wakati itakua inaonekana dhahiri kwamba picha hiyo imefifia.
Kwa sasa mtandao wa WhatsApp uko katika hatua za mwanzo kabisa katika kuhakikisha kuwa wanalikomesha hili jambo –picha haitakiwi kupungua ubora wake wakati wa kutumwa.
Ni kwa muda tuu watu na wataalam mbalimbali hawatumii mtandao huu kama sehemu ya kutumia picha mfano picha za maharusi n.k na badala yake hutumia huduma zingine kama vile barua pepe n.k
Kitakacho fanyika ni kwamba wakati wa kutuma picha hizo mdau atatakiwa kuchagua ubora (quality) anaotaka –na utaendana una utumiaji wa data—ila kuutuma kwa mtu.
Kwa taarifa zinazopatiikana katika mtandao wa WABetaInfo ni kwamba mtu ataweza kuchagua machaguo ya ‘Standard Quality’ na ‘HD Quality’’
Lakini hili lilionekana muda tuu maana kumbuka kulikua na ongezeka kubwa la ukubwa wa mafaili yanayotumwa ndani ya mtandao huu yaani kutoka 100MB mpaka 2GB ni wazi kabisa tatizo la picha kupungua ubora lazima lingeondoka tuu.
Huduma hii itaanza kupatika kwenye WhatsApp zote yaani ile App ya kwenye simu na hata pia katika WhatsApp ya mtandao yaani WhatsApp Web.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hii umeipokeaje? Na je wewe ni muhanga wa kupoteza ubora wa picha kupitia katika mtandao huu wa kijamii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.