WhatsApp huwa wanatoa maboresho kadha wa kadha ilimradi kuhakikisha kwamba wanazidi kuwaletea huduma bora watumiaji wake.
Licha ya WhatsApp kuwa na vipengele vingi vya aina yake lakini bado wana mpango wa kuja na mengine mengi na lililotufikia hivi karibuni ni kwamba mtandao huo unakuja na kipengele kingine katika maswala ya Ulinzi (security).
Hapa mtandao una mpango wa kuja na kipengele ambacho kitakuwezesha kufungia chat zake kadhaa katika eneo moja ambalo ili kuzifikia lazima uweke neno siri –au hata utumie alama za vidole (finger print)—ilimradi kufikia mazungumzo hayo.
Kumbuka kwa sasa ndani ya App ya WhatsApp mtu anaweza ku’lock WhatsApp nzima kwa kutumia neno siri/alama za vidole/utambulizi wa sura.
Lakini kwa kutumia kipengele hiki kipya ataweza kufanya hivyo kwa baadhi ya mazungumzo (chats) na kingine kizuri ni kwamba hata picha/video katika mazungumzo haya hazitaenda moja kwa moja katika Gallary ya kawaida.
Kwa sasa kipengele hiki kiko katika majaribio na kionyesha dhahiri kina hati hati kubwa sana ya kuanza kupatikana rasmi kwa watu wote kutokana na uhitaji wake kuwa wa hali ya juu.
Ukifikiria sana utagundua chat za aina hii zitakua zinaonekana katika eneo lingine kabisa yaani kama zile chat za Archives zinavyokua zimejitenga.
Ni wazi kwamba WhatsApp wana mambo mengi sana ambayo yatakuja na yote hili ni katika kulihakikishia soko kwamba wao ndio wanatoa huduma bora kabisa kulinganishwa na wengine.
Chanzo:WABetaInfo
Ningependa kusikia kutoka kwako, je wewe unadhani kipengele hiki ni kizuri sana na kitakuasaidia sana? Au unadhani ibakie kama ilivyo tuu na Ku’lock iwe kwa App yote?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.