WhatsApp mwisho kupatikana kwenye baadhi ya simu za zamani kuanzia hivi karibuni.
Kama bado unatumia simu ambayo imeingia sokoni miaka kadhaa nyuma basi fahamu huu ni muda wa kubadilisha kama unataka kuendelea kutumia WhatsApp.

WhatsApp mwisho kupatikana kwenye simu zifuatazo;
- Simu zinazotumia programu endeshaji ya Windows – itakapofika Disemba 2019
- Simu za iPhone zinazotumia toleo la iOS 7 na matoleo ya nyuma – itakapofika Februari 1 2020
- Simu za Android (Samsung, Tecno, Huawei n.k) zinazotumia toleo la Android 2.3.7 na matoleo ya miaka ya nyuma – itakapofika Februari 1 2020
Microsoft tayari walishaacha kutengeneza simu zinazotumia programu endeshaji ya Windows miaka zaidi minne iliyopita na kwa simu za Android watengenezaji wengi walishasasisha (update). Ila inasemakana bado kuna watumiaji kadhaa wanaotumia simu zenye matoleo ya Android ya zamani kutumia huduma ya WhatsApp.
Tayari WhatsApp walikwisha acha kutengeneza matoleo mapya (masasisho/updates) ya app hii kwa ajili ya matoleo haya ya programu endeshaji (OS).
Huu ni muendelezo wa kuondoa huduma hii kwa programu endeshaji ambazo hazina sifa za kuwa salama tena kutokana na kutopata masasisho.
Soma habari zaidi za app ya WhatsApp – Teknokona/WhatsApp