Kipindi ambacho Facebook ilinunua WhatsApp mwaka 2014 kwa dola za kimarekani bilioni 19, watu wengi na wadau wa teknolojia walikuwa na swali moja la kujiuliza nalo ni Kwa nini Facebook wamenenua mtandao huo?
Hakukuwa na sababu ya Facebook na WhatsApp kumilikiwa na mtu mmoja na kuwa chini ya kampuni ya Facebook. Lakini hata hivyo kulikuwa na baadhi ya maeneo yanayoonyesha kuwa hizi mbili kidogo zinaendana.
Kwa taratibu Facebook inaonyesha kuwa inashughulika katika kuziweka Facebook na WhatsApp karibu
Taarifa iliyovuja ni kwamba katika toleo jipya la WhatsApp kutakuwa na ruhusa ya mawasiliano kati ya mtandao wa Whatsapp na mtandao wa Facebook . Wataalamu walipokuwa wakicheza na teknolojia ya kuroot simu katika Android waligundua kuwa toleo la whatsApp lile la 2.12.413 lilionyesha kuwa kuna chaguo la kuunganisha WhatsApp na Facebook kwa lengo la ‘kukuza uzoefu wa kutumia Facebook’
Licha ya kuwa matumizi kamili ya maunganisho haya bado hajajulikana kwa uhakika. Inaweza ikawa kwamba whatsapp inawaruhusu watumiaji wake kuweza kupost vitu Facebook wakiwa katika WhatsApp. Au pengine matumizi sahihi ya muunganiko huu yatajulikana pale muungano huu utakapoanza kufanya kazi.
Lakini pia kitu kimoja ambacho ni cha uhakika ni kwamba kwa kipindi kijacho mtumiaji wa WhatsApp atakuwa na uwezo wa kupost katika mtandao wake wa Facebook na WhatsApp akiwa katika moja ya mitandao hiyo.
Mtandao wa WhatsApp ambao ndio mkubwa katika App zile za kutuma na kupokea meseji imeripotiwa kuwa mtandao huo upo katika matayarisho ya kuweza kutumia mtandao huo kupiga simu za kuonana uso kwa uso kama vile Skype. Lakini pia kumbuka ilipiga chini tozo zake za mwaka (dola 0.99)
Tuambie wewe unahisi nini ambacho unakitarajia kutokea kutokana na muunganiko huu, tuandikie sehemu ya comment hapo chini. Pia usisahau kutembelea mtandao wako pendwa wa teknokona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!
Vyanzo: GSMArena na vyanzo vinginevyo
No Comment! Be the first one.