Kwa sasa katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp ukiwa umetuma ujumbe kimakosa basi huna lingine la kufanya zaidi ya kuufuta tuu.
Hili linaenda kubadilika maana kwa sasa kuna kipengele kinafanyiwa kazi na kazi kubwa ya kipengele hiki ni kuhakikisha kuwa haufuti meseji yako yote ndani ya mtandao huo wa WhatsApp.
Kwa wengi kipengele hichi cha kufanya uhariri sio kipya na katika mitandao mingi ya kijamii –mfano facebook na instagram — huwa kinapatikana kuanzia katika sehemu ya kuandika ‘caption’ na hata katika eneo la ‘comment
Vyanzo mbalimbali vinasema kuwa kipengele hiki kwa mara ya kwanza kabisa kitaanza kupatikana katika vifaa vya iPhone na kisha pengine labda kinaweza kuhamia katika Android.
Hili la kuanza kupatikana katika iPhone linachangiwa pia na toleo la iPhone 14 kuingia katika soko huku likiwa na kipengele hiki katika jumbe zake za iMessage.
Kupitia chanzo cha kuaminika kabisa ambacho mara kwa mara kimekua kikitoa taarifa za mwanzo kabisa kuhusiana na vipengele vingi vya whatsApp-WABetaInfo, kimeonesha screenshot ya kipengele hicho.
Mpaka sasa haiku wazi kuu ya lini kipengele hiki kitaanza kupatikana katika vifaa husika na kipo katika hatua za mwanzo kabisa.
Tutaendelea kukujuza kwa kile kinachotufikia kuhusiana na kipengele hiki ikiwemo siku ya kuachiwa kwake n.k.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ulikua unasubiria kwa hamu kipengele kama hichi? Au kwako wewe uwezo ule ule wa kufuta kabisa jumbe ambazo umezifuta.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.