Hebu pata picha ndani ya mtandao wa WhatsApp ukawa umemtumia mwenzio ujumbe kisha ukaufuta lakini baada ya kuufuta tuu ukagundua kuwa umefanya makosa, hukutakiwa kufanya hivyo.
Pengine hilo litakua na suluhisho hivi karibuni maana vyanzo mbalimbali vinasema kuwa mtandao wa WhatsApp unakuja na kipengele ambacho kitakua na uwezo wa kufufua ujumbe uliofutwa.

Kwa sasa kampuni imekua ikifanya maboresho na kuongeza vipengele mbalimbali, hivi karibuni tuliandika kuhusiana na mtandao huo kuweza kuongeza muda wa kufuta jumbe katika mtandao huo, soma zaidi >>HAPA<<
Kitakachotokea hapa ni kwamba wakati umefuta ujumbe huo kutakua na ujumbe unaoelea ukisema UNDO, kama utachagua ujumbe huo basi ujumbe wako utarudi.

Kwa sasa ni mitandao mingi tuu ambayo ina teknolojia ya aina hii nadhani kama ni mtumiaji wa Gmail mara kwa mara utakua umeshakutana na kipengele cha UNDO.
Kwa sasa kipengele hiki kipo kwenye majaribio na nadhani hivi karibuni tuu kitaanza kupatikana kwa watumiaji wote wa mtandao huo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini je kwa upande wako kipengele hichi kitakusaidia kwa namna moja au nyingine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.