WhatsApp leo wamewatangazia watumiaji wake juu ya maboresho waliyoyafanya ambapo kwa sasa si wao (WhatsApp) wala mitandao ya simu/serikali itaweza kuona chats au kusikiliza maongezi ya watu wanaotumia huduma hiyo.
Kupitia teknolojia inayofahamika kama end to end encryption maboresho hayo yameifanya huduma hiyo ya WhatsApp kuwa moja ya app zenye usalama zaidi kama vile Telegram na iMessage iliyo kwa watumiaji wa iOS.
Kupitia end to end encryption data zote zinazopita katika huduma ya WhatsApp hufichwa kwa password spesheli kwenye app ya mtumiaji na kishwa kusafirishwa huku ikiwa ni data isiyoweza someka kwa mtoa huduma wa intaneti na mitambo ya WhatsApp na kisha data hizo zinapopokelewa kwa mlengo app ya mtumiaji hiyo itasoma data hizo na kuzionesha kwa mtumiaji.
Mazungumzo ya aina yote yatakuwa salama – kuchati na pia ata kupiga simu
Suala la usalama wa data dhidi ya wadukuzi wa aina mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na vyombo vya usalama vya kiserikali limekuwa jambo lililopewa kipaumbele sana na makampuni ya simu na watoa huduma za kimtandao. Uamuzi huu wa WhatsApp umepewa pongezi sana na watu wote wanaopigania haki ya usiri ya watumiaji wa huduma hizo.