Baada ya kuwa inapatikana bure kwa muda mrefu kwa simu za Android Whatsapp imeanza kutolewa bure kwa iPhones pia.
Kabla ilikuwa ni lazima mtumiaji ainunue kwa dola za kimarekani 0.99 ila kwa sasa mtumiaji ataweza kuishusha bure na kutumia kwa muda wa mwaka mmoja na baada ya hapo itabidi kufanya malipo ya dola moja kwa mwaka au kuchagua malipo mengine ya miaka mingi zaidi.
WhatsApp imezidi kupata wapinzani wengine katika huduma hii kama vile Viber, WeChat na Line, lakini bado hakuna iliyoweza kufikia usawa kwa idadi ya watumiaji. Whatsapp ilizinduliwa mwaka 2009 na hadi sasa imezidi kuwa maarufu na kwa sasa kila mwezi inatumiwa na takribani watu milioni 250 na takribani ujumbe mfupi bilioni 27 hutumwa kila mwezi. Idadi hii ya ujumbe mfupi ni zaidi ata ya idadi ya ‘Tweets’ zinazotumwa Twitter kila mwezi.
Kushusha WhatsApp kwenye iPhone yako bofya hapa, kwa Android unaweza kubofya hapa!
No Comment! Be the first one.