Baada ya takribani miezi miwili tangu WhatsApp Web ilipowasili kwenye kivinjari cha Google Chrome, huduma hiyo sasa inapatikana kwenye vivinjari vya Mozilla Firefox na Opera.
WhatsApp walitoa tangazo hilo kupitia akaunti yao ya twitter.
WhatsApp Web ni kioo cha WhatsApp ya kwenye simu za mkononi inayomuwezesha mtu kufanya mawasilano ya WhatsApp kupitia kompyuta na hivyo kuokoa muda wa kuokota simu.
Kama umeshasoma makala yetu ya kufungua WhatsApp haraka zaidi kwenye Chrome na unajiuliza utafanya vipi kwenye Firefox, usiwe na shaka. Hapa tuna ufumbuzi.
Firefox
- Ingia kwenye Firefox.
Fungua web.whatsapp.com. - Upande wa kushoto, kabla tu ya anuani utaona alama ya Dunia au nembo ya tovuti. Ishikilie hiyo alama na uiburuze kwenda kwenye eneo-kazi lako na uiachilie hapo.
- Tayari utakuwa umeweka njia ya mkato ya kufika haraka zaidi kwenye WhatsApp hapo.
Je, wewe unafanyaje kufika kwenye WhatsApp kirahisi zaidi kwenye Opera au hata vivinjari vya Chrome na Firefox? Tujuze kupitia mitandao yetu ya facebook, instagram na twitter au barua pepe, mhariri@teknokona.com .
No Comment! Be the first one.