Tunaishi katika wakati ambao teknolojia inashika kasi sana na kugusa watu wa kila aina katika kila kona za dunia. Makampuni yanafanya maamuzi tofauti kuendana na jambo hili na moja ya mifano hii ni uamuzi huduma ya WhatsApp kuongeza rangi tofauti ya ngozi kwenye vikatuni vya maongezi.

Si lazima sasa, kutumia vikatuni vya rangi ya iliyozoeleka kwenye WhatsApp na badala yake utaweza kuchagua rangi unayotaka kati ya rangi 5 zaidi kwa sura na sehemu zingine za kibinadamu. Unachotakiwa kufanaya ni kubofya moja ya vikatuni vya aina hii, shikilia na achia, alafu chagua rangi unayotaka. Hiyo itakuwa rangi yako kwa vikatuni vinginevyo mpaka utakaporudia zoezi hilo tena.

Kipengele hiki kimekuwepo kwenye ‘WhatsApp Web’ kwa muda mrefu na sasa kipo katika majaribio kwenye vifaa vya Androidi na unaweza kujipatia kwa kushusha na kupakia WhatsApp ‘beta’ moja-kwa-moja kutoka kwenye kurasa maalumu ya WhatsApp. Kwa wale wenye vifaa vingine kama Windows Phone na i-phone, huduma hii ipo pia.
Jambo la ziada na muhimu kujua ni kwamba vikatuni hivi vipya vitaweza kuonekana na mtu mwingine anayetumia WhatsApp beta kwa sasa.

Picha Na: IBNLive
No Comment! Be the first one.