Watumiaji wa Android na wa huduma za WhatsApp na Viber wamerahisishiwa zaidi kutuma ujumbe wa pupa, kama wanajua kutumia kipengele cha ‘OK Google’ kwenye Google Now.
Kipengele hichi cha OK Google kinatumika kuamuru simu ya Android na hata kivijari cha Google Chrome kufanya mambo kadha wa kadha. Kwenye simu yako kwa mfano, unaweza kuitumia kutafuta vitu kwenye Google, kuweka alamu, kuandika SMS na barua-pepe, kupiga simu na kadhalika.
Mapema mwaka huu, Google ilitangaza kwamba itaruhusu app zingine kutumia uwezo wa Google Now kurahisisha matumizi ya Simu yako. Sasa, Google Now inaweza kutumika kutuma ujumbe sio tu kwa WhatsApp na Viber, bali hata kwa WeChat, NextPlus na Telegram pia. Unachotakiwa kufanya ni kusema kitu kama ‘OK Google’, ‘Send WhatsApp message to Eric,’ alafu utaulizwa ujumbe unaotaka kutuma. Sema ujumbe wako na ujumbe wako utakuwa umetumwa. Unaweza kuangalia video hapo chini.
Hata hivyo, kuanza kutumia WhatsApp kwenye simu yako, yakupasa kusasisha WhatsApp pamoja na app ya Google na kuiwezesha simu yako kutumia ‘OK Google’ kwenye mipangilio ya app ya Google. Ilani: Lugha ambayo inatumika kwa sasa ni kiingereza na lugha nyingine chache zilizokomaa kwenye kipengele cha ‘OK Google’.
No Comment! Be the first one.