Kama ni mtumijai mzuri wa WhatsApp web —WhatsApp ile ya njia ya mtandao katika kompyuta — bila shaka ulikua huwezi hata kumtumia mawasiliano kwa mtu ambao unawasiliana nae sio?
Katika mtandao wa WhatsApp ni rahisi sana kutuma mawasiliano ya mtu mwingine wakati unawasiliana na mwingine sio? Jambo ambalo lilikua linashindikana katika WhatsApp Web.
Ni wazi kwamba huduma ya WhatsApp Web ilikua haina vipengele vingi ukilinganisha na ambavyo vinapatikana katika App ya kawaida.
Mtandao wa WhatsApp umekua katika mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inawafanya watumiaji wa iOS, Android Na hata Windows kuwa wanasubiri kwa hamu vipengele vipya vitakavyoongezwa katika mtandao huo.
Mara kwa mara tumekua tukikuandikia vipengele kadha wa kadha ambavyo huwa vinawekwa kwa njia ya masasisho na mtandao huu wa kijamii.
Huduma hii itakuasaidia kufika katika kitabu chako cha mawasiliano (contact book) kwa haraka na kuweza kuchagua mawasiliano ambayo unataka kumtumia mtu ndani ya mtandao huo.
Kwa sasa huduma hii inapatikana kwa baadhi ya watu ikiwa ni kama sehemu ya majaribio lakini itaanza kupatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp ya mtandaoni hivi karibuni.
Toleo hili ni mahususi kwa watumiaji wa WhatsApp Web na wale wanaotumia Microsoft Store katika kuhakikisha kuwa wanapata App ya WhatsApp.
Wanaotumia majukwaa mengine wataendelea kama kawaida maana wao huduma hiyo wamekua wakiifurahia kwa kipindi cha muda mrefu sasa.
CHANZO: WaBetaInfo
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, umeshawahi kutumia WhatsApp Web? Je hii umeipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.