WhatsApp ni moja kati ya huduma ya kurahisisha mawasaliano duniani na ni moja kati ya mtandao ambao una watumijiaji wengi kabisa katika kila pande ya dunia.
Mara kwa mara mtandao huo wa WhatsApp umekua ukileta vipengele na masasisho (update) mapya ili kuhakikisha kwamba watumiaji wao wanapata huduma bora kabisa.
Kuna huduma yao ya WhatsApp Web ambayo inaruhusu kutumia huduma hiyo katika web, huku huduma hiyo ikiwa ni kama kioo kwa huduma ile ya kwenye simu.
Lakini cha kushangaza ni kwamba kuna baadhi ya vitu unaweza kuvifanya katika ile ya simu lakini ukashindwa fanya katika ile ya mtandao.
Moja ya kitu ni kama ule uwezo wa kutuma jumbe/video/picha katika status ya WhatsApp kwa kutumia huduma WhatsApp Web.
Katika WhatsApp Web beta version 2.2353.59 (toleo la majaribio) imeonekana dhahiri kwamba jambo hili litawezekana hivi karibuni.
Hii ni moja kati ya njia za kufanya huduma hii isiwe na utofauti wa utumikaji katika maeno yote mawaili yaani ile ya kawaida na hata katika Web.
Kwa sasa ni wazi kwamba kipengele hiki kipo katika majaribio na kinatumika kwa baadhi ya watu waliochaguliwa.
Mambo yakikaa sawa basi kipengele hiki kinaweza kikaanza kutumika kwa watu wote ili kuweza kufurahia huduma hii.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sehemu ya comment je unadhani hili litafanya watumiaji wa huduma hii kuongezeka zaidi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.