Unaweza kusema WhatsApp ndio programu tumishi ambayo inafanyiwa maboresho mengi kuzidi nyingine nyingi tuu ambazo tunazifahamu/kuzisikia. Mpangilio wa namba za watu waliopo kwenye WhatsApp kwa sasa umekaaje?
Kwenye ulimwengu huu wa teknolojia ni muhimu sana kufanya vitu viwe ni rahisi kupatikana. Wakati fulani watu walilalamikia mtindo mpya wa mpangilio kwa kuziweka katika makundi ya watu unaowasiliana mara kwa mara, uliowasiliana nao hivi karibuni. Mpangilio huo haukupendwa na wengi na kutaka namba zao za simu kwenye WhatsApp zipangiliwe kwa kufuata mtiririko wa herufi (A-Z) lakini pia ionekane idadi ya jumla ya namba za simu wanaotumia programu hiyo tumishi.
Kufuatia malalamiko ya watu mbalimbali WhatsApp imesikia na kuamua kurudisha mtindo uleule wa mwanzo ambao umeonekana kuwavutia watumiaji wengi wa programu tumishi husika ambayo inapata watumiaji wapya kila siku.
Kwa mujibu wa WhatsApp wameshaanza kupeleka masasisho na hivyo kuwezesha watuaji kurudi kule walipotoka. Hii inafuatia baada ya watumiaji wa WhatsApp kulalamikia mtindo mpya wa mpangilio wa namba za simu.
Mabadiko hayo pia yanakwenda hata kwenye Android na iOS na hata WhatsApp ya kutumika kwenye kompyuta ,Je, wewe ni mmoja kati ya wale waliobahatika kuona ile sura mpya?
Vyanzo: WaBetaInfo, mitanao mbali
No Comment! Be the first one.